Wikimapia is a multilingual open-content collaborative map, where anyone can create place tags and share their knowledge.

Visiwa vya Virgin vya Marekani | archipelago (en)

Virgin Islands (US) / Saint John / Cruz Bay /
 archipelago (en), invisible (en)
 Upload a photo

Visiwa vya Virgin vya Marekani (United States Virgin Islands) ni visiwa katika Bahari ya Karibi ambavyo ni visiwa chini ya Marekani, wakazi ni raia wa Marekani lakini hawashiriki katika uchaguzi wa Rais wala wa bunge la Washington DC. Viko takriban 80 km upande wa mashariki ya Puerto Rico.

Ni sehemu ya funguvisiwa vya Visiwa vya Virgin iliyogawiwa kati ya Uingereza na Marekani. Kisiwa cha Saint John cha Marekani ni karibu sana na kisiwa cha Tortola upande wa Kiingereza. Pande zote mbili za funguvisiwa kuna ushirikiano wa kiuchumi zikitumia dollar ya Marekani.

Ni hasa visiwa 4 vya St. Thomas, St. John, St. Croix na Kisiwa cha Maji (Water Island) pamoja na visiwa vingi vidogo.

Eneo lao kwa jumla ni 346.36 km². Sensa ya mwaka 2002 ilihesabu wakazi 108,612.

Visiwa hivi ni sehemu ya pekee ya Marekani ambako magari yanatembea upande wa kushoto ya barabara.

Visiwa vilikuwa koloni ya Denmark vikauzwa 17 Januari 1917 kwa Marekani.
Nearby cities:
Coordinates:   18°2'30"N   64°48'42"W
  •  778 km
  •  1739 km
Array