Visiwa vya Virgin vya Uingereza
British Virgin Islands /
Tortola /
Road Town /
World
/ British Virgin Islands
/ Tortola
/ Road Town
/ Visiwa vya Virgin vya Marekani
archipelago (en), invisible (en), British oversea territory (en)
Visiwa vya Virgin vya Uingereza (British Virgin Islands) ni visiwa katika Bahari ya Karibi karibu na Puerto Rico ambavyo ni eneo la ng'ambo la Uingereza. Wakazi ni raia wa Ufalme wa Muungano (Uingereza) lakini hawashirikiani katika uchaguzi wa bunge la London.
Katika sehemu hii ya nyororo ya Visiwa vya Bikira (Virgins) kuna visiwa 16 vyenye wakazi na zaidi ya 30 visivyo na watu. Eneo lake ni 153 km². Idadi ya wakazi hufikia takriban 22,000. Wengi wao (85-90%) ni wa asili ya Kiafrika; mababu walikuwa watumwa kutoka Afrika waliopelekwa visiwani kwa kazi kwenye mashamba ya miwa.
Visiwa vikubwa ni Tortola, Virgin Gorda, Anegada na Jost Van Dyke. Mji wa pekee na makao makuu ya kiutawala ni Road Town kwenye kisiwa cha Tortola.
Uchumi hutegemea zaidi utalii. Menginevyo kuna ushirikiano wa kiuchumi na sehemu ya Kimarekani ya visiwa vya Virgins na pesa inayotumika hata upande wa Kiingereza ni dolari ya Marekani.

Wikipedia article: https://sw.wikipedia.org/wiki/Visiwa_vya_Virgin_vya_Uingereza
Nearby cities:
Coordinates: 18°31'43"N 64°33'33"W
Array